A). Vocabulary |
kosi [course] ratiba [schedule] ratiba ya kila siku [daily schedule] desturi; shughuli [routine] desturi/shughuli za kila siku [daily routine] robo [quarter] semesta [semester] muhula[term] hadi/mpaka[until] |
B). Daily Schedule [ratiba ya kila siku] |
[7:00 am - 8:00 am] Saa moja asubuhi hadi/mpaka saa mbili asubuhi:Huamka, hunawa uso, huoga na hula chakula cha asubuhi au hunywakahawa.[I wake up, wash my face, shower, and eat breakfast or drink coffee.] [8:00 am - 12:00 pm] Saa mbili asubuhi hadi/mpaka saa sita mchana:Huenda darasani, na husoma darasani.[I go to class, and I study in class.] [12:00 pm - 1:00 pm] Saa sita mchana hadi/mpaka saa saba mchana:Hula chakula cha mchana na hulala kidogo.[I eat lunch and sleep a little.] |
[2:00 pm - 4:00 pm]
Saa nane mchana hadi/mpaka saa kumi mchana:Huenda/hurudi darasani tena.
[I go/return to class again.]
[5:00 pm - 7:00 pm]
Saa kumi na moja jioni hadi/mpaka saa moja usiku:Hucheza, hukimbia, hufanya mazoezi, na huenda kazini.[I play, run, work out, and go to work.]
[7:00 pm - 8:00 pm]
Saa moja usiku hadi/mpaka saa mbili usiku:Hula chakula cha jioni na huenda kwenye filamu.[I eat dinner and go to a movie.]
[8:00 am - 9:00 pm]
Saa mbili usiku hadi/mpaka saa tatu usiku:Hufanya kazi ya nyumbani na huenda mkutanoni.[I do homework and go to a meeting.]
[9:00 pm - 12:00 am]
Saa tatu usiku hadi/mpaka saa sita usiku:Husoma historia/Kiswahili, hufanya marudio na pia hupiga nguo pasi.[I study history/Kiswahili, I do a review and iron clothes.]
[12:00 am - 6:00 am]
Saa sita usiku hadi/mpaka saa kumi na mbili alfajiri:Hupumzika nyumbani mwangu na hulala hadi/mpaka asubuhi.[I rest at my house and sleep until morning.]
Question Formation |
Mifano: |
1. Wewe hufanya nini kila siku?[What do you do every day?] a). Mimi hufanya mambo mengi kila siku kwa mfano: ______.[I do a lot of things every day, for example: ______.] b). Mimi huenda filamuni. [I go to a movie.] c). Mimi huenda mkutanoni. [I go to a meeting.] d). Mimi huenda michezoni. [I go to games.] 2. Ratiba yako ni gani semesta hii?[What is your schedule this semester?] a). Semesta hii ratiba yangu ni: [This semester my schedule is:] b). Ratiba yangu semesta hii ni: [My schedule this semester is:] 3. Unafanya kosi gani semesta hii?; Semesta hii unafanya kosi gani?[What courses are you taking this semester?] a). Semesta hii ninafanya kosi nyingi kwa mfano/kama/kama vile Kiswahili…[This semester I am taking many courses for example/like/such as Kiswahili...] b). Ninafanya kosi nyingi kwa mfano/kama/kama vile Kiswahili… [I am taking many courses for example/like/such as Kiswahili...] 4. Unasoma nini semesta hii/semesta hii unasoma nini?[What are you studying this semester?] a). Semesta hii ninasoma Kiswahili,historia[This semester I am studying Kiswahili, history.] b). Semesta hii nina kazi nyingi sana. [This semester I have a lot of work] c). Semesta hii nina kazi kidogo.[This semester I have little work.] d). Sisomi masomo yoyote.[I am not taking any studies.] 5. Mimi ninapenda/sipendi semesta hii kwa sababu...[I like/don’t like this semester because...] |
No comments:
Post a Comment